Aunty Ezekiel hataki lawama

Tuesday May 15 2018

 

By MYOVELA MFWAISA

MWIGIZAJI mkali wa filamu Bongo, Aunty Ezekiel amesema hafurahishwi na maneno maneno kutoka kwa wasanii wenzake hasa linapotokea jambo ambalo linahitaji mmoja wao kusaidiwa au kuzikwa kwani, mambo hayo hukatisha tamaa watu wanaojitoa.

Aunty alisema siku zote huwa hapendi lawama na mtu kwani kuna wengine huwa ni vimbelembele kutaka kuwaharibia wenzao siku tu.

“Mambo ya ajabu sana unakuta msanii hata hajulikani na hana msaada wowote Bongo Movie, lakini ndio kimbelembele wa kuwalaumu waliojitoa mfano huyo Rammy alitoa kiasi gani?” alisema Aunty.

Msanii huyo alisema hayo baada ya sakata lililomkumba Mwenyekiti wa Bongo Movie, Steven Nyerere ikisemekana alishindwa kuwakilisha michango ya rambirambi kwa mtoto wa Masogange.

Baadaye Rammy Galis aliibuka akisema atauza filamu zake kwa ajili ya kumsaidia mtoto huyo, ndipo Aunty akahoji ametoa kiasi gani?