Mambo 4 yanayomfanya Diamond asishuke kimuziki

Muktasari:

  • Vigezo hivi vimemwezesha kuwa katika levo tofauti na wasanii wengine katika ukanda huu na ndio sababu Tanzania brandi yake hiyo aliyojitengenezea imemwezesha kuwa msanii mwenye  dili nyingi za matangazo na pia asiyekosa shoo.

Mwanamuziki Diamond Platinumz amejijengea brandi ya kuuzika kupitia ubora wa kazi zake, staili yake nadhifu ya fasheni, skendo za kiki, kolabo kadhaa na wasanii wa kimataifa kama vile Omarion, Davido, Neyo na wengine.

Vigezo hivi vimemwezesha kuwa katika levo tofauti na wasanii wengine katika ukanda huu na ndio sababu Tanzania brandi yake hiyo aliyojitengenezea imemwezesha kuwa msanii mwenye  dili nyingi za matangazo na pia asiyekosa shoo.

Lakini pia brandi yake hiyo imemwezesha kuvutia makampuni ya nje kufanya kazi naye. Alipokuja kuzindua albamu yake Kenya. Kampuni ya Safaricom iliwahi na kumlipa zaidi ya KSh5 milioni kushirikiana naye kwenye uzinduzi wake huo jambo ambalo lililowaumiza wasanii wengi wa Kenya.

Ubora wake umemfanya kutumika sana na Safaricom kwenye shoo zao.

Diamond ana timu nzima inayoshughulika na usanii wake kuanzia kwa madansa, Ma-DJ, wapiga picha, mameneja watatu wanaomsaidia kuendesha lebo yake.

Kwa shoo za nje ya nchi, Diamond huchaji kiasi kisichopungua Dola 40,000 kwa shoo za nje ya nchi.

2015 kwenye shoo ya ‘Kiboko Yao’ kwenye Ukumbi wa ‘Leader Club’ Tanzania,  Diamond alilipwa Tsh100 milioni (Sh4.4 milioni)  kiasi alichosema kuwa kikubwa zaidi kuwahi kulipwa kwa shoo ya nyumbani.