Zari: Tumeachana kabisa na Diamond

Muktasari:

Wawili hao wamefanikiwa kupata watoto wawili kabla ya kuvunjika kwa uchumba huo

Dar es Salaam. Zari ‘The Boss Lady' amesema hafikirii na hatarajii kurudiana na mzazi mwenzake Diamond Platnums huku akisisitiza 'tumeachana kabisa.'

Zari aliyezaa na Diamond msanii maarufu ndani na nje ya nchi watoto wawili ameyasema hayo jana Februari 23,2018 alipokuwa akihojiwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC).

"Nilikaa sana muda mrefu nikafikiria vitu vingi ndio nikasema unajua nini nahitaji kufikia mwisho wa hili," alisema Zari alipoulizwa na mtangazaji Marian Omary kuhusu ujumbe wake aliouweka katika akaunti yake ya kijamii ya Instagram wa alioelezea kuachana na mzazi mwenzake.

Alipoulizwa ulikaa na kutafakari ukaona ufikie hili, Zari amejibu "Tulikuwa tunajaribu kuona tuna 'move'  kutoka  hiyo 'scandal' (kashfa) ya kuwa amepata mtoto na tunaweza kusonga mbele."

"Lakini vitu kama hivi leo unasikia ivi leo unaona vile sijui kukumbatiana na ma X katika public, vitu vya kunidhalilisha, kunifanya nisiheshimike  watoto wangu," ameongeza

Alipoulizwa kama Diamond alimpigia simu kumuomba msamaha baada ya picha hizo kusambaa Zari amesema hakufanya hivyo na wala yeye hakuona haja ya kumpigia simu kumuuliza.

Kuhusu Diamond kama atakwenda kumwomba msamaha atakubali Zari amesema "si alishakuja kipindi  fulani alipozaa na huyo dada fulani (Hamisa Mabeto) sioni kama itawezekana."

Kama Diamond ametuma watu wa kukwombea msamaha Zari alisema hawezi kulizungumzia hilo kwa kujibu 'no comment'.

Alipoulizwa kama ni kiki za wao kuachana Zari amejibu "yaani tumeachana kabisa, 'it's done'. sijui kama amekubali, tangu video zile zimetoka na X wake nimempiga block wiki tatu hatuongei ndio nikawa nimepost."