Yanga yatua uwanjani kuisubiri Njombe Mji

Muktasari:

Yanga inashuka dimbani leo kucheza mechi ya pili katika mzunguko wa pili huku ikiwa imeanza vyema mechi ya kwanza dhidi ya Lipuli FC.

Dar es Salaam. Kikosi cha Yanga, kimetua uwanja wa Taifa na kuanza mazoezi mapesi mchana huu kwa ajili ya mechi yao dhidi ya Njombe Mji jijini Dar es Salaam, leo Jumanne.

Yanga inashuka dimbani leo kucheza mechi ya pili katika mzunguko wa pili huku ikiwa imeanza vyema mechi ya kwanza dhidi ya Lipuli FC.

Kocha Msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa amesema kikosi chake kipo tayari kuivaa Njombe Mji baada ya kazi nzito ya Iringa dhidi ya Lipuli.

Yanga inashuka uwanjani ikiwa na majeruhi wa kadhaa kwenye kikosi chake ambao watalazima kuitazama timu yao wakiwa benchi.