Mbwembwe zaiponza Yanga mechi ya Lipuli

Tuesday February 13 2018

 

By Eliya Solomon

Dar es Salaam. Klabu ya Yanga imetozwa faini ya  Sh1 milioni  kwa kutotumia malango rasmi sawa na Lipuli katika mchezo huo na kutotumia vyumba vya kubadilishia nguo.
Katika kudhibiti tabia za kutotumia vyumba vya kubadilishia nguo, Mtendaji mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura amesema wameandaa mpango maalumu ambao anaamini utakuwa na tija.
“Hizi timu zimekuwa zikidai kuwa kwenye hivyo vyumba sijui kuna dawa. Sasa msimamizi wa mchezo husika ambaye ndiye kamishina wa mechi atawajibika pia kutuandikia ripoti ya kuonyesha sababu hizo husika,” alisema.
“Bodi pia itaandaa utaratibu maalumu wa kuthibitisha hayo ambayo yamekuwa yakisemwa,” alisema mtendaji huyo mkuu wa Bodi ya Ligi,” alisema kiongozi huyo.
Wambura aliongeza kwa kusema mbali na kuwa wanakagua viwanja kwa kuzingatiwa ubora wa sehemu ya kuchezea, wataanza kutazama katika upande wa uzio na maeneo muhimu kama vyumba vya kubadilishia nguo.