Yanga yaisogelea Simba

Dar es Salaam.Timu ya Yanga imeifunga Ruvu Shooting bao 1-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo Jumapili.

Ushindi huo wa Yanga unaipandisha hadi nafasi ya tatu wakifikisha pointi 25, pia wakiisogela Simba iliyopo nafasi ya pili huku Azam wakipanda kileleni baada ya kuifunga Prisons kwa mabao 2-0.

Bao lililofungwa na Pius Buswita limepunguza presha iliyokuwa imetanda kwa mashabiki na viongozi wa Yanga iwapo wangepoteza mchezo huo.