Yanga mambo yao mbele kwa mbele

Muktasari:

Yanga imefanikiwa kufuzu kwa robo fainali ya Kombe la FA

Dar es Salaam. Mshambuliaji wa Yanga, Emmanuel Martin amesema pamoja na kupata ushindi wa mabao 2-1 ugenini dhidi ya Majimaji mechi ilikuwa ngumu.

Martin mfungaji wa bao la pili la Yanga alisema Majimaji ilikuwa vizuri na kukiri kwamba ni uzoefu ndio uliwafanya washinde mechi hiyo na kufanikiwa kutinga robo fainali ya Kombe la FA.

"Majimaji waliupiga mwingi kiasi kwamba tusingekuwa makini basi tungekuwa tunaongea mengine, laiti kama wangekuwa wanaonyesha ushindani huo kwenye ligi wangekuwa pazuri zaidi," alisema Martin.

Mshambuliaji huyo alizungumzia ratiba ya Ligi Kuu kwamba inawafanya wachoke kwani sasa wapo safari kuelekea Mtwara kucheza mechi dhidi ya Ndanda.

"Tunachoka ila hatuna budi kuendelea kupambana kwani ndio imeishakuwa, tunachokiangalia ni Yanga kwanza mengine baadae, tunashukuru tunafanikiwa kwa sehemu," alisema mshambuliaji huyo.