Yanga waenda kulipa kisasi Botswana

Muktasari:

Yanga na Township watacheza Jumamosi hii mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa ni
mchezo wa marudiano wa raundi ya pili baada ya ule wa kwanza waliocheza Dar es Salaam na  watoto hao wa Jangwani walifungwa kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Taifa mbao 2-1.

MSAFARA wa Yanga ambao ni wachezaji 20 pamoja na viongozi 1,  wameondoka alfajiri ya
leo saa 10:15 na ndege ya Ethiopia kwenda Botswana kuivaa Township.
Yanga na Township watacheza Jumamosi hii mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa ni
mchezo wa marudiano wa raundi ya pili baada ya ule wa kwanza waliocheza Dar es Salaam na  watoto hao wa Jangwani walifungwa kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Taifa mbao 2-1.
Wachezaji waliondoka ni pamoja na Mcameroon Youthe Rostand, Ramadhani Kabwili, Juma
Abdul, Gadiel Michael, Nadir Haroub 'Cannavaro', Pato Ngonyani, Said Juma 'Makapu', Kelvin Yondani 'Vidic',  Mkongo Papy Tshishimbi na  Abdallah Shaibu.
Mzimbabwe Thabani Kamusoko, Juma Mahadhi, Andrew Vincent 'Dante',  Mzambia Obrey Chirwa, Geofrey Mwashiuya, Raphael Daud, Yussuph Mhilu,  Emmanuel Martin, Pius Buswita na Ibrahim Ajib.
Benchi la ufundi ni pamoja na makocha Wazambia George Lwandamina na Noel Mwandila, Shadrack Nsajigwa, Juma Pondamali, Hafidh Saleh, daktari wa timu Edwin Pavu, Jacob Onyango, Mahamood Omary 'Mpogolo'  pamoja na viongozi,  Omary Kaya, Samwel Lukumay na Elius Mwanjala.