Kocha wa St. Louis aikana Yanga

Muktasari:

"Ni mara yetu ya kwanza kuja hapa, hatujawahi kuja japa,  Yanga wenyewe tumewajulia kupitia mtandao wa CAF.

Kocha wa St Louis, Michel Renald ameikaushia Yanga wanaocheza nao Jumamosi ya wiki hii, huku akidai kwamba hakuna anachojua juu ya wapinzani wake hivyo anaamini mechi itakuwa ngumu.
"Ni mara yetu ya kwanza kuja hapa, hatujawahi kuja japa,  Yanga wenyewe tumewajulia kupitia mtandao wa CAF.
Hivyo mchezo utakuwa mgumu kwa sababu sizani kama wao wenyewe wanatufahamu sisi, "alisema.
Akizungumzia kuhusu kutuma wawakilishi katika mchezo wa Yanga dhidi ya Njombe Mji, alisema hana uhakika na suala hilo ila alipata taarifa ya ushindi wa wapinzani wao hao ambao watakipiga nao siku ya Jumamosi.
"Sisi tumeingia hapa usiku sana hatukuweza kuiona hiyo mechi, lakini tulipata matokeo ya wapinzani wetu kwamba wameshinda, wamefanya vizuri kupata ushindi na sisi ndio tunaendelea na mazoezi, "alisema.