Wapinzani wa Yanga wapiga mazoezi Uwanja wa Karume

Dar es Salaam. Kikosi cha St Louis ambacho kinashuka dimbani Jumamosi dhidi ya wenyeji Yanga, kimefanya mazoezi yake leo Jumatano kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam

Yanga inaliwakilisha Taifa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika CAF mchezo wa kwanza utakaopigwa dhidi ya  St. Louis ya Shelisheli.

Timu hiyo ya visiwani, imewasili jana Jumanne usiku na leo asubuhi wamefanya mazoezi uwanja wa Karume. Chanzo cha taarifa kilieleza kwamba kikosi hicho kimewaka kambi yao Kariakoo.

Kikosi cha Yanga kinajiandaa na mchezo huo kwa ujasiri baada ya kufanya vyema mechi zake tatu za  hivi karibuni za Ligi Kuu.