Wanyama aitwa Liverpool kuzipa pengo la Can

Muktasari:

  • Kiungo huyo Mkenya alikuwa nje ya uwanja kwa muda akisumbuliwa na majeruhi

Liverpool imeanza kumtolea macho kiungo wa Tottenham Spur, Victor Wanyama kuwa mrithi wa Emre Can.

Gazeti la Daily Mail limedai kuwa kocha Jurgen Klopp anamtaka Wanyama kuziba pengo la Can ambaye mkataba wake unaenda mwishoni.

Wanyama (26), amekuwa katika wakati mgumu kupata namba katika kikosi cha kwanza cha Spurs chini ya kocha Mauricio Pochettino ambaye anapenda kuwatumia zaidi Mousa Dembele na Eric Dier.

Lakini kiungo huyo Mkenya amebaki kuwa moja ya viungo bora wa kabaji kwa sasa katika Ligi Kuu England.

Kwa sasa Mjerumani Can anaweza kuondoka kama mchezaji huru kwenda Juventus mwisho wa msimu baada ya  kumaliza mkataba wake na miamba hiyo ya Anfield.

Pia, wanakaribia kumsajili Naby Keita kutoka RB Leipzig baada ya kufikia makubaliano.

Hata hivyo, nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard anaamini Klopp anahitaji kumsajili mbeba maji, ambaye atawaruhusu viungo wengine kuendelea kushambulia.

Amemtaja Wanyama kwamba ndiye mtu sahihi, Gerrard alisema: “Nafikiri Liverpool watafaidika zaidi wakiwa na kiungo mkabaji.

 “Wanyama ni aina mchezaji anayeweza kucheza kwa nidhamu katika kuhakikisha anaongeza ulinzi katika safu ya mabeki wanne.