Wamasai wamkuna Rais wa Fifa

Muktasari:

Rais wa Fifa alikuwa nchini kwa mkutano wa siku moja wa Shirikisho hilo la soka duniani

Dar es Salaam.Kati ya mambo ambayo Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa, Fifa, Gianni Infantino yamemvutia ni wamasai pamoja na kuvalishwa mgolole.

Akizungumza baada ya mkutano uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jana, Infantino alieleza kufurahishwa na ukarimu wa Watanzania akisema hajawahi kukutana na kitu hicho.

"Nimefurahi, kukutana na Maasai...," alisema Infantino na kuamsha kicheko kwa waandishi wa habari.

Mara baada ya kuwasili kwenye ukumbi huo asubuhi, alipokewa na ngoma ya wamasai kutoka Ngorongoro mkoani Manyara ambao walimvika mgolole wa kimasai, Infantino na Rais wa CAF, Ahmad Ahmad.

Alisema: "Tumekuja Tanzania tumefurahishwa na mengi. Kwanza tumekuja kuangalia hali ya soka kwa baadaye, na ninashukuru mambo yamekwenda kama yalivyopangwa.

"Lengo la kuja Tanzania ni kuangalia soka yetu kwa baadaye, kupanga mammbo ya maendeleo ya soka na Tanzania ni kwa sababu hatutaki kuifanya soka iwe Zurich pekee.

"Tunaileta soka kwa wanasoka wenyewe, miaka ya nyuma mikutano ya Fifa ilikuw aikifanyika huko, lakini sasa tutaitawanya dunia nzima, tulikuwa Nigeria na sasa tuko Tanzania."