St Louis yatua Uwanja wa Taifa kuziona Simba, Azam FC

Muktasari:

Kikosi cha St Louis ambacho kinashuka dimbani Jumamosi dhidi ya wenyeji Yanga, kimefanya mazoezi yake leo Jumatano kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.

Wachezaji wa St. Louis wamefika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kushuhudia mechi ya Simba na Azam inayoendelea jioni hii leo Jumatano.
Kikosi cha St Louis ambacho kinashuka dimbani Jumamosi dhidi ya wenyeji Yanga, kimefanya mazoezi yake leo Jumatano kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.
Wachezaji hao walionekana jukwaani wakifuatilia kwa ukaribu mechi ya Simba na Azam ambayo imekuwa na ushindani mkali kutokana na kufukuzana kwenye msimamo wa Ligi Kuu.
Yanga inaliwakilisha Taifa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika CAF mchezo wa kwanza utakaopigwa dhidi ya  St. Louis ya Shelisheli.
Timu hiyo ya visiwani, imewasili jana Jumanne usiku na leo asubuhi wamefanya mazoezi uwanja wa Karume. Chanzo cha taarifa kilieleza kwamba kikosi hicho kimewaka kambi yao Kariakoo.
Kikosi cha Yanga kinajianda na mchezo huo kwa ujasiri baada ya kufanya vyema mechi zake tatu za  hivi karibuni za Ligi Kuu.