VIDEO: Yanga yapata mapokezi makubwa Songea

Muktasari:

Mabingwa hao wa Tanzania Bara wanakibarua kizito katika kuhakikisha wanaendelea kubaki katika Kombe la FA

Songea. Wachezaji wa Yanga wamewasili mjini Songea mkoani Ruvuma mchana wa leo na kupata mapokezi makubwa kutoka kwa mashabiki wao kabla  ya mchezo wao wa kesho wa Kombe la Shirikisho 'FA' dhidi ya wenyeji Majimaji 'Wanalizombe'.

Yanga imewasili katika Hotel ya Ugabe katikati ya mji wa Songea saa 8:20 mchana wakiwa katika basi wakitokea Uwanja wa Ndege wa mjini Songea na kupokewa kwa shangwe na ndelemo za mashabiki wake waliofurika hotelini hapo.

Mashabiki wa Yanga wameonakana kujawa na furaha wakati wakiipokea timu yao huku wakiimba na kucheza na wengine wakizungumza mitaani kwa pikipiki zao.

Yanga itawakabili 'Wanalizombe' hao kwenye Uwanja wa Majimaji kesho.