Ulimwengu asubiri kibali kucheza Bosnia

Dar es Salaam. Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Ulimwengu anategemea kujiunga klabu ya FK Sloboda Tuzla ya nchini Bosnia and Hezgovina.

Ulimwengu aliachwa na AFC Eskilstuna ya Sweden kutokana na kuwa na majeraha sugu ya goti, hatimaye ndoto yake ya kucheza Ulaya inakaribia kukamilika kwa kujiunga na klabu ya FK Sloboda.

Meneja wa mchezaji huyo, Jamal Kasongo alisema kwa sasa Ulimwengu anasubili kupata kibari cha kufanyakazi katika nchi hiyo, lakini aligoma kutaja ni timu gani atajiunga nayo.

Hata hivyo siri ya Ulimwengu kupata nyingine imejulikana baada ya kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga kumwita katika kikosi chake kitakachocheza mechi mbili za kirafiki katikati ya mwezi huu.

Taifa Stars wataanza kwa kucheza ugenini dhidi ya Algeria Machi 22, 2018 na siku tano baadaye watareja nchini kuwakabili DR Congo Machi 27, 2018 Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.