Ulimwengu amerudi mwanangu

Muktasari:

  • Meneja wa mchezaji huyo, Jamal Kassongo alisema wapo kwenye hatua za mwisho za kukamilisha kibali chake cha kazi ambacho kitamwezesha kuanza rasmi kuichezea timu hiyo ya Ligi Kuu nchini humo.

SIKU chache zijazo huenda winga wa Taifa Stars, Thomas Ulimwengu akaanza kukinukisha katika klabu yake mpya ya FK Sloboda Tuzla inayoshiriki Ligi Kuu nchini Bosnia and Herzegovina.

Meneja wa mchezaji huyo, Jamal Kassongo alisema wapo kwenye hatua za mwisho za kukamilisha kibali chake cha kazi ambacho kitamwezesha kuanza rasmi kuichezea timu hiyo ya Ligi Kuu nchini humo.

“Watanzania wamekuwa na shauku ya kutaka kusikia maendeleo ya Ulimwengu, yupo na hiyo timu na anaendelea na program zao mbalimbali, vielelezo vyake vimetumwa tayari.

“Ile ni nchi ya watu, wana taratibu zao ambazo mimi na wewe hatuzifahamu, kila kitu kitakuwa sawa kwenye hizi siku mbili tatu,” alisema Kasongo.

Klabu hiyo imekiri kukamilisha taratibu za usajili wa Ulimwengu na sasa wanachosubiri ni kukamilika kwa kibali hicho ili aanze kucheza.