NMB yaongeza neema Azam FC

Muktasari:

Afisa Mtendaji wa Azam FC, Abdul Mohammed alisema tangu waanze kudhaminiwa na benki hiyo, wamekuwa wakifanya vizuri katika timu yao.

Dar es Salaam. KLABU ya Azam FC imeingia mkataba wa mwaka mmoja na Benki ya NMB, ambapo mkataba huu unakuwa ni wa mwaka wa nne mfululizo.
Afisa Mtendaji wa Azam FC, Abdul Mohammed alisema tangu waanze kudhaminiwa na benki hiyo, wamekuwa wakifanya vizuri katika timu yao.
"Wamekuwa karibu na sisi kwa muda mrefu, wamechangia katika soka letu la vijana, tuna vijana saba mpaka hivi sasa katika timu kubwa, jambo jema kwa sababu nao wanahusika katika hili," alisema.
Mkurugenzi wa NMB, Ineke Bussemaker alisema wanavutiwa na maendeleo ya klabu ya Azam, hiyo ndio sababu ya wao kuwekeza katika klabu hiyo.
"Ni timu ambayo inatuwakilisha vyema katika mashindano ambayo inashiriki, tunawapongeza kwa kuchukua ubingwa wa Mapinduzi Cup kwa sababu wameitangaza nchi vizuri, tumeshakuwa nao kikazi lakini ni zaidi ya ndugu, " alisema.