Tshishimbi ambwaga Okwi tuzo ya mchezaji bora

Dar es Salaam. Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limemtangaza Papy Kabamba Tshishimbi  kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu Tanzania  Bara, mwezi Februari huku akiwabwaga  Pius Buswita na Emmanuel  Okwi.

TFF ilitangaza tuzo hiyo ya mchezaji bora wa mwezi huu wakati Msemaji wa shirikisho hilo ali[pokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Jumanne.

Tshishimbi ambaye ni raia wa Congo, amesafiri na kikosi cha timu yake kwenda Botswana kwa ajili ya mchezo wa marudiano na Township Rollers.

Kiungo huyo wa Yanga, timu yake imefikisha pointi 46 kwenye msimamo wa Ligi Kuu sawa na Simba iliyopo kileleni wakiwa na tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.