Township Rollers yaiwekea ngumu Yanga

Dar es Salaam. Timu ya Yanga imeshikwa nyumbani baada ya kukubali kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Township Rollers kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika mechi iliyochezwa Uwanja wa Taifa leo Jumanne.

Bao la Yanga limefungwa na Obrey Chirwa dakika ya 30 huku mabao ya Township yakifungwa na Lemponye Tshreletso (11) na Motsholetsi Sikele dakika ya 83.

Matokeo hayo yanaiweka Yaga kwnye nafasi ngumu kutokana na kutakiwa kupata ushindi wa kuaniza mabao 2-0 wataka[okwenda kwenye mechi ya marudiano nchini Botswana.