Tenga aainisha faida ujio rais wa Fifa

Tuesday February 13 2018

 

Dar es Salam. Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania BMT, Leodegar Tenga amezungumzia umuhimu wa ujio wa Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa hapa nchini.


Alisema moja ya sababu ya ujio wao ni kutoka na  kutambua Watanzania wapenda mpira.
Hivyo ujio wao utakuwa na msaada mkubwa wa kuendelea soka la vijana wanawake na klabu.


Tenga alisema kila hatua ambayo rais wa Fifa atakuwa hapa itakuwa inamulikwa na dunia hivyo ni vyema tukawapokea vizuri.


Ujio wake rais wa fifa pia watakuja hapa kupanga agenda za mkutano mkuu wa Fifa.


Awali, Waziri Mwakyembe  alisema ujio huu rais wa Fifa ni heshima kwa Taifa hivyo vyombo vya habari vina wajibu wa kutangaza nchi.


"wanapotoka Nigeria wakija hapa tuwaonyeshe utofauti, kwa sababu wanaweza kutufanyia mambo makubwa kama ilivyokuwa kwa majirani zetu Rwanda.


Naamini hata rais TFF atapanga mpango mzuri kwa waandishi wa habari  ili wasiachwe nyuma kama ilivyokuwa ujio wa Everton.


Rais TFF, Wallace Karia alisema kutakuwa na utaratibu maalumu kwa wanahabari.
Tutazungumza na wenzetu wa Fifa juu ya utaratibu wa wanahabari kwa kuangalia mfumo wao.