Stand United waja na mbwembwe za kuwafunga Yanga

KATIBU  wa Stand United 'Chama la Wana',Kenny Nyangi amesema licha ya ratiba kuwabana na kujikuta wanatumia muda mwingi kusafiri, watahakikisha wanailiza Yanga katika mechi watakayocheza Jumatatu.
Nyangi anasema kama waliweza kutoka sare ya mabao 3-3 na Simba, hajaona kinachoweza kuwazuia kuwafunga Yanga ambao wanaonekana hawako kwenye fomu nzuri kwa msimu huu.
"Uwezo wetu utaheshimika kupitia klabu hizo kongwe,ambazo ndizo zinaonekana zina timu bora kuliko nyingine katika Ligi  Kuu Bara,"
"Tunahitaji kujikwamua kushuka daraja, wachezaji wameishaamka na wanajua wanataka nini,kama viongozi tumehakikisha wapo vizuri kuelekea mchezo huo,tutapambana na si kufungwa na Yanga,"anasema.