Zlatan, Rojo pigo Man United

Muktasari:

Katika mchezo huo mshambuliaji mkongwe Zlatan Ibrahimovic akitolewa nje baada ya kuumia goti jambo linalozua hofu kuwa Mswedeni huyo huenda akawa nje hadi mwisho wa msimu huu. 

Jose Mourinho ameishudia Manchester United ikipamba kufuzu kwa nusu fainali ya  Europa Ligi, lakini hakuna ushindi usiokuwa na kilio. 

Katika mchezo huo mshambuliaji mkongwe Zlatan Ibrahimovic akitolewa nje baada ya kuumia goti jambo linalozua hofu kuwa Mswedeni huyo huenda akawa nje hadi mwisho wa msimu huu. 

Ibrahimovic alidondoka baada ya kujaribu kuunganisha mpira kama alivyokuwa mapema  Marcus Rojo na wote kuondolewa uwanja wakiwa majeruhi.

Katika mchezo huo Man United ilifanikiwa kusonga mbele baada ya kushindi mabao 2ñ1 na kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-2 dhidi ya Anderlecht.

Kiungo Henrikh Mkhitaryan alifunga bao la kwanza kabla ya Marcus Rashford kufunga bao la pili katika dakika 107.