Zidane kuteuliwa kocha wa Ufaransa

Muktasari:

Zidane ambaye ni raia wa Ufaransa, timu yake imenyakua taji la La Liga msimu huu jambo lililompandisha kwenye viwango vya ubora.

 Baada ya kunyakua taji la ubingwa msimu huu, Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane ana nafasi kubwa ya kuteuliwa kuongoza timu ya Taifa ya Ufaransa kwenye mashindano ya Kombe la Dunia mwakani.

Zidane ambaye ni raia wa Ufaransa, timu yake imenyakua taji la La Liga msimu huu jambo lililompandisha kwenye viwango vya ubora.

Kocha huyo ana kibarua kingine ambacho kitahitimisha iwapo anafaa kuwa Kocha wa Ufaransa. Ushindi katika mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa huenda ukampa sifa zaidi ya kuwa kuwa kocha bora Hispania na barani ulaya msimu huu.

Zidane aliwahi kunyakua tuzo ya mchezaji bora wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) mara tatu. Pia amewahi kuichezea Real Madrid tangu mwaka 2001-2006. Januari mwaka alichukua nafasi ya ukocha kuifundisha klabu hiyo.