Zidane ampa tano Ronaldo kuukaribia ubingwa

Hispania. Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane amesifu kiwango cha mshambuliaji wa kikosi hicho, Cristiano Ronaldo kutokana na kiwango cha juu alichoonyesha msimu huu.

Zidane alisema kwamba mchezaji huyo amekuwa na msimu mzuri hata kuiwezesha timu hiyo kuukaribia ubingwa wa La Liga msimu huu.

Ronaldo aliifungua timu yake bao wakati kalbu hiyo ilipoiadhibu Celta Vigo kwa mbao 4-1 jana Jumatano na kusogea pointi tatu dhidi ya wapinzani wao Barcelona.

Hata hivyo Ronaldo anakaribia kuweka rekodi nyingine ya kuwa mfungaji bora wa ligi tano za barani Ulaya msimu huu.