Yaya aitwa benchi la ufundi

Muktasari:

Kiungo huyo mwenye miaka 33 alitangaza kustaafu soka kucheza soka la kimataifa tangu Septemba mwaka jana baada ya kuichezea Ivory Coats michezo 113.

Kocha mpya wa timu ya Taifa ya Ivory Coast aliyeteuliwa hivi karibuni, Marc Wilmots amesema anataka kumtumia Yaya Toure katika benchi lake la ufundi.
Kiungo huyo mwenye miaka 33 alitangaza kustaafu soka kucheza soka la kimataifa tangu Septemba mwaka jana baada ya kuichezea Ivory Coats michezo 113.
“Nimetazama michezo miwili ya mwisho aliyoichezea Manchester City katika safu ya ulinzi ya kiungo. Amekuwa akifanya vizuri bado ana uwezo mkubwa,” Wilmots aliwaeleza waandishi  wa habari.
Nitakwenda kuonanana naye na nitazungumza naye kuhusu suala hilo. Ninatambua umuhimu wake kwa kuwa ni mchezaji mwenye uzoefu mkubwa. Nadhani bado mchango wake unahitajika nitamshawishi arudi kushirikiana nasi. Suala la Yaya Toure nitalipa kiaumbele,” alisisitiza.
Kocha huyo raia wa Ubelgiji (48) amewahi kuifundisha timu ya taifa hilo iliyoshiriki mashindano ya Euro 2016 na sasa ameingia mkataba na Shirikisho la Soka cha Ivory Coast.
“Sina uzoefu sana kuhusu nchi hii lakini nina taarifa za kutosha kuhusu timu hii ya taifa na nilikuwa natamani kufundisha timu ya taifa,” alisema.
Hii ni timu yenye wachezaji wengi vijana  kwa ajli ya baadaye. Naweza kusema kwamba hiki ni kizazi cha dhahabu. Wakati shirikisho liliponipa nafasi nikajihoji kwa nini isiwezekane?”
Wilmots anatarajiwa kukinoa kikosi hicho hadi mwaka mwaka 2019 kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) na kwenye mashindano ya fainali za Kombe la Dunia.