Yanga yaikamia Prisons Kombe la FA

Muktasari:

Mwambusi  alisema wamejiandaa kuhakikisha wanashinda mchezo huo na kujiweka katika nfasi nzuri ya kutetea ubingwa wao.

Dar es Salaam. Kocha msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi amesema rekodi hizo hazina nafasi katika mchezo wao  wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) kesho dhidi ya Prisons  kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mwambusi  alisema wamejiandaa kuhakikisha wanashinda mchezo huo na kujiweka katika nfasi nzuri ya kutetea ubingwa wao.

"Mbali na ubingwa, pia hii ni njia ya kushiriki mashindano ya kimataifa msimu ujao, hivyo tunajua umuhimu wa mchezo  huu. Tutawapa heshima yao na wala hatutowadharau.

"Tutawakosa wachezaji wawili kutokana na majeraha hapo kesho ambao ni Vicent Bossou na Donald Ngoma" alisema kocha huyo wa zamani,  Mbeya City.

Tayari Simba, Azam na Mbao zimeshafuzu kwa nusu fainali ambayo ratiba yake itapangwa Jumapili Aprili 23 katika ofisi za Azam zilizopo Tabata.

 

xxxxxxxxxx