Yanga wakutana kumjadili Manji

Muktasari:

Manji alitangaza kujiuzulu nafasi hiyo jana Jumanne kwa alichodai kushauriwa na daktari wake kupumzika.

Dar es Salaam. Viongozi wa matawi wa klabu ya Yanga Mkoa wa Dar es Salaam wamekutana leo Jumatano kujadili barua ya kujiuzulu  ya Mwenyekiti wa klabu hiyo Yusuph Manji.

Manji alitangaza kujiuzulu nafasi hiyo jana Jumanne kwa alichodai kushauriwa na daktari wake kupumzika.

Mwananchi limeshuhudia kikao hicho kikiendelea makao makuu Mtaa wa Jangwani huku waandishi wakizuiwa kuingia.

Kikao hicho kinachoongozwa na Katibu Mkuu, Charles Mkwasa kitafuatiwa na kikao kingine cha kamati ya utendaji baadaye leo na kitaamua kuridhia au kutoridhia barua ya kujiuzulu kwa Manji.

Manji aliyeingia Yanga kama mfadhili tangu mwaka 2006, ameiongoza klabu hiyo akiwa mwenyekiti tangu 2012 baada ya kujiuzulu kwa Lyoid Nchunga.