Willian hatari kwa mipira iliyokufa

Wednesday April 19 2017

 

By London, England

Nyota wa Chelsea, Willian, Pedro na Michy Batshuayi  walikuwa wakifanya mazoezi ya kushinda kufunga wakati timu yao ikijindaa na mechi ya nusu fainali ya Kombe la FA dhidi ya Tottenham Spurs.

Watatu hao walikuwa wakishinda kufunga kutoka  kona mbalimbali goli kama walivyokuwa wakielekezwa na kocha Allan Russell aliyekuwa akiangalia uwezo wao wa kufunga.

Baada ya ushindani mkali na kulingana kwa ufungaji, mtaalamu wa mipira iliyokufa, Willian alionyesha tofauti yake kwa kufunga kwa mpira wa adhabu uliowaacha midomo wazi wenzake.

Antonio Conte alikuwa akiwaandaa wachezaji wake hao hasa baada ya Tottenham kuwasogelea kileleni wakiwa nyuma yao kwa tofauti ya pointi nne.

Kipigo ilichopata Blues kutoka kwa Manchester United mwisho wa mwa wiki hasa baada ya kiungo Ander Herrera kufanikiwa kumfunika Eden Hazard katika mchezo huo.

Hivyo Willian na Pedro wanahitaji kwa haraka kuanza kama watakutana na timu nyingine inayocheza aina ya uchezaji wa Man United.