Wenger azitosa Chelsea, Man City

Muktasari:

  • Badala yake, ameeleza kuwa  yuko radhi kumwachia aondoke kama mchezaji huru mwishoni mwa mkataba wake, 2018 kuliko kumuuza kwa wabaya wake, Chelsea au Manchester City msimu ujao.

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amesema safari hii yuko makini, hayuko radhi kumwachia mshambuliaji wake, Alexis Sanchez aende kwa wapinzani wake, Chelsea na Manchester City zinazomtaka.
Badala yake, ameeleza kuwa  yuko radhi kumwachia aondoke kama mchezaji huru mwishoni mwa mkataba wake, 2018 kuliko kumuuza kwa wabaya wake, Chelsea au Manchester City msimu ujao.
Wenger,  ambaye wiki hii alieleza matumaini ya kumshawishi mshambuliaji huyo raia wa Chile kusaini mkataba mpya baada ya kuiwezesha kukata tiketi ya kucheza fainali ya Kombe la FA dhidi ya Chelsea mwezi ujao, alieleza kuwa hawezi kumuuza kwa gharama yoyote, tena kwa wabaya wake.
Alieleza kuwa hawezi kurudia makosa ya kuuza mchezaji wake muhimu kwa wapinzani wake, kama alivyowahi kufanya kwa Robin van Persie kwenda kwa Manchester United.
ìHata Sanchez  hatasaini mkataba mpya kwa sasa, niko tayari kumwachia kama mchezaji huru, lakini siwezi kumuuza kwao;î alieleza Wenger.
Aliongeza kuwa kila dalili inaonyesha kuwa mshambuliaji huyo mwenye miaka 28 atasaini mkataba mpya licha ya mazungumzo baina ya pande hizo kukwama kwa sasa.