http://www.mwanaspoti.co.tz/image/view/-/3894660/medRes/1619783/-/8k3r1sz/-/pic+wenger.jpg

Soka

Wenger afikiria kumaliza ëtop fourí England

Share Bookmark Print Email
Email this article to a friend

Submit Cancel
Rating

 

By London, England  (email the author)
Email this article to a friend

Submit Cancel


Posted  Jumanne,Aprili18  2017  saa 19:19 PM

Kwa ufupi;-

Mabao kutoka kwa Alexis Sanchez na Mesut Ozil yalitosha kuwapa pointi tatu Gunners katika mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Riverside. Pia, kipindi cha pili Alvaro Negredo aliipatia timu yake bao.

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ameibuka na kuanza tambo baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Middlesbrough juzi.

Mabao kutoka kwa Alexis Sanchez na Mesut Ozil yalitosha kuwapa pointi tatu Gunners katika mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Riverside. Pia, kipindi cha pili Alvaro Negredo aliipatia timu yake bao.

Ushindi huo umewapa nguvu mpya kwenye mbio za kumaliza katika nafasi nne za juu kwenye Ligi Kuu England inayoelekea ukingoni.

Timu hiyo imebakiza pointi saba ili kuipiku Manchester City inayoshika nafasi ya nne. Hata hivyo kikosi hicho cha Guardiola kina michezo mingi ukilinganisha na Arsenal yenye mchezo mmoja mkononi.

Kocha huyo raia wa Ufaransa amekiri,  awali walianza kupoteza mwelekeo baada ya kupokea kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Crystal Palace wiki iliyopita.

ìNilihisi kwamba tulikuwa na mipango. Kama mlivyoona hatukucheza kwa kujiamini lakini kiuhalisia tulihitaji ushindi,î alizungumza Wenger wakati akihojiwa na Sky Sport.