Wanariadha watatu kusaka utajiri Marekani

Muktasari:

Mbio hizo za viwanjani zinazotarajia kufanyika Jumatatu Mei 29 katika mji wa Colorado, wanariadha wa Tanzania watakaoshiriki mbio hizo ni Ismail Juma, Gabriel Gerald na Josephat Joshua.

Arusha. Wanariadha watatu wa Tanzania wanatarajia kuondoka nchini kesho kwenda  Marekani kushiriki mbio za km 10 zijulikanazo kama  Bolderbolder 

Mbio hizo za viwanjani zinazotarajia kufanyika Jumatatu Mei 29 katika mji wa Colorado, wanariadha wa Tanzania watakaoshiriki mbio hizo ni Ismail Juma, Gabriel Gerald na Josephat Joshua.

Katibu mkuu wa Shirikisho la Riadha (RT), Wilhem Gidabuday amesema mbio hizo ni fursa wa wanariadha hao kunyakua kujitangaza zaidi pamoja na kujipatia fedha nyingi iwapo watashinda.

ôHao ni wanariadha waliofikia viwango vya kushiriki mbio za kimataifa hivyo mbali na fursa ya kuchukua kitita, pia watumie kuwasoma wenzao ambao watakutana nao katika mbio za dunia ili kujua mbinu zao. 

Mwanariadha Ismail Juma amesema huu ni mwaka wa mafanikio kwake hivyo hawezi kufanya vibaya hata mara moja

ôMbali na kuwakilisha nchi na kurejesha heshima ya riadha kwa Tanzania, lakini ni fursa kwangu kutoka kimaisha kwa fedha za zawadi zinazotolewa kwa washindi hivyo lazima nijitahidi nishinde.ö

Mwanariadha Juma alinyakua kitita cha dola 35,000 (sawa na zaidi ya Sh 70milioni), baada ya kushinda mbio æVodafone Istanbul half marathonÆ zilizofanyikia nchini Uturuki mwezi uliopita.

Kocha wa mwanariadha Josephat Joshua, Rogath Steven amesema ni mara chache mwanariadha wake kushiriki mbio kubwa kama hizo hivyo amelazimika kumpa mazoezi ya ziada ili arudi na ushindi.