Wachina wakanusha kumtaka Costa

Muktasari:

Uongozi wa klabu hiyo ulifafanua kwamba ndani ya miezi sita iliyopita hawajawahi kukaa mezani kuzungumza na Costa.

Beijing, China. Klabu ya Tianjin Quanjian wamesisitiza hawajafanya mazungumzao na mshambuliaji wa Chelsea kuhusu uhamisho wake kwenda Ligi ya China.

Uongozi wa klabu hiyo ulifafanua kwamba ndani ya miezi sita iliyopita hawajawahi kukaa mezani kuzungumza na Costa.

Raia huyo wa Hispania, amekuwa akihusishwa kwenda kucheza sokaa Ligi Kuu ya China.

Hata hivyo kwa taarifa zilizopo, baada ya Chelsea kutwa taji la ubingwa msimu huu, mchezaji huyo ataendelea kuwapo kikiosini hapo kwa msimu mwingine ujao.

Vyombo vya habari hivi karibuni vilitoa taarifa kwamba, Costa ametangaziwa dau la Pauni 60 milioni.

Kocha Antonio Conte alisema yupo tayari kumruhusu mchezaji kuondoka klabuni hapo iwapo hana dhamira ya kuitumikia timu hiyo.