UAMUZI WA ADHABU MBALIMBALI KUTOKA KAMATI YA SAA 72

Muktasari:

Klabu ya Yanga imepigwa faini ya sh. 1,000,000 (milioni moja) kutokana na timu yake kutoingia vyumbani wakati wa mechi hiyo iliyochezwa Mei 9, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

UAMUZI WA ADHABU MBALIMBALI KUTOKA KAMATI YA SAA 72

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) litavuna mamilioni ya shilingi kutoka na faini mbalimbali ilizotozwa klabu kutokana adhabu za Kamati ya Saa 72.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TFF leo inaonyesha klabu za Yanga, Mbao zimeongoza kwa kutozwa fainali kutokana na makosa mbalimbali waliyoyafanya wachezaji pamoja na mashabiki wao katika mechi za mwisho wa msimu huu.

Uamuzi wa adhabu hizo ni kama ifuatavyo:

Mechi namba 206 (Yanga 1 Vs Toto Africans 0).

Klabu ya Yanga imepigwa faini ya sh. 1,000,000 (milioni moja) kutokana na timu yake kutoingia vyumbani wakati wa mechi hiyo iliyochezwa Mei 9, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 14(48) ya Ligi Kuu. Uamuzi huo umezingatia pia kuwa Yanga imekuwa ikirudia kosa hilo mara kwa mara.

Mechi namba 225 (JKT Ruvu 0 Vs Majimaji 1).

Timu ya Majimaji haikuingia vyumbani wakati wa mapumziko katika mechi hiyo iliyofanyika Mei 13, 2017 katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Kutokana na timu hiyo kurudia kufanya kosa hilo, klabu ya Majimaji imepigwa faini ya sh. 1,000,000 (milioni moja). Adhabu hiyo ni uzingativu wa Kanuni ya 14(48) ya Ligi Kuu.

 

Mechi namba 230 (Kagera Sugar 2 Vs Mbao FC 0).

 

Klabu ya Mbao imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na timu yake kutoingia vyumbani wakati wa mechi hiyo iliyochezwa Mei 13, 2017 katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. Adhabu hiyo ni uzingativu wa Kanuni ya 14(48) ya Ligi Kuu.

 

Mechi namba 231 (Yanga 2 Vs Mbeya City 1).

 

Timu zote mbili hazikupita kwenye mlango rasmi wakati wa kuingia uwanjani katika mechi hiyo iliyochezwa Mei 13, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Hivyo, kila klabu imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na kitendo hicho, uamuzi ambao umezingatia Kanuni ya 14(48).

Pia, klabu ya Yanga imepigwa faini ya sh. 1,000,000 (milioni moja) kwa kutoingia vyumbani kwenye mechi hiyo. Adhabu hiyo pia imezingatia Kanuni ya 14(48) ya Ligi Kuu.

 

Mechi namba 236 (Mbao FC 1 Vs Yanga 0).

Klabu ya Yanga imepigwa faini ya sh. 1,000,000 (milioni moja) kwa kupita mlango usio rasmi katika mechi hiyo iliyofanyika Mei 20, 2017 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(48) ya Ligi Kuu.

 

Pia, Yanga imepigwa faini ya sh. 1,500,000 (milioni moja na laki tano) kwa kutoingia vyumbani. Adhabu hiyo imezingatia Kanuni ya 14(8) ya Ligi Kuu. Vilevile klabu hiyo imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na kuonyesha vitendo vinavyoashiria ushirikiana. Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 42(1) ya Ligi Kuu.

Washabiki wa Yanga walivunja uzio wa ndani (fence) wa upande wa Magharibi wakati wakiingia uwanjani kusherehekea ubingwa wa timu hiyo. Hivyo, klabu ya Yanga imeagizwa kulipa gharama za uharibifu huo uliofanywa na washabiki wake, uamuzi ambao umezingatia Kanuni ya 42(3) ya Ligi Kuu.

 

Nayo klabu ya Mbao FC imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na washabiki wake kuingia uwanjani kushangilia baada ya timu yao kupata ushindi.