Tshabalala ampiku Niyonzima uchezaji bora

Muktasari:

Hussein aliwashinda wachezaji Haruna Niyonzima wa Yanga na Shabani Idd wa Azam FC.

Dar es Salaam. Beki wa Simba SC, Mohamed Hussein 'Tshabalala' amekuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom wa mwezi Mei kwa msimu wa 2016/2017.

Hussein aliwashinda wachezaji Haruna Niyonzima wa Yanga na Shabani Idd wa Azam FC.

Katika mwezi Mei kulikuwa na raundi tatu ambazo Hussein alicheza kwa dakika zote 270 na kutoa mchango mkubwa katika kuisadia timu yake kubaki katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom.

Pia, alionesha nidhamu ya hali ya juu, hivyo kutopewa onyo la aina yoyote.

Kwa kushinda tuzo hiyo, Hussen atazawadiwa kitita cha sh. 1,000,000 (milioni moja) kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya Vodacom Tanzania.

Wachezaji wengine walioshinda tuzo za mwezi za Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2016/2017 ni John wa Mwadui (Februari), Mbaraka Yusuf wa Kagera Sugar (Machi) na Abdulrahman Musa wa Ruvu Shooting (Aprili).Bocco wa Azam (Agosti), Shiza Kichuya wa Simba (Septemba), Simon Msuva wa Yanga (Oktoba) na Riphat Said wa Ndanda (Novemba).

Wengine ni Method Mwanjali wa Simba (Desemba), Juma Kaseja wa Kagera Sugar (Januari), Hassan Kabunda