Tanzania yapanda nafasi tano Fifa

Saturday December 20 2014

By MWANDISHI WETU

TANZANIA imepanda kwenye chati za ubora wa soka wa Dunia kwa nafasi tano kutoka 105 hadi 110. Hiyo ni kwa mujibu wa chati mpya iliyotolewa na Fifa Jana Ijumaa.

Katika jedwali hilo la ubora, Ujerumani inaongoza dunia ikifuatiwa na Argentina na Colombia. Kwenye nchi za ukanda wa Afrika Mashariki, Uganda ni ya 84, Kenya ya 116, Rwanda ya 95 na Burundi ni ya 128.

Tanzania imekuwa ikipiga hatua taratibu kwenye chati hiyo kutokana na timu yake ya Taifa kushindwa kufanya vizuri kwenye michuano mingi ya kimataifa.