Tanzania, Uganda kundi moja kufuzu Afcon 2019

TAIFA STARS

Muktasari:

Katika droo iliyochezeshwa jana usiku jijini Libreville, Gabon, mbio za kusaka tiketi ya kufuzu fainali hizo zitaanza Juni mwaka huu na kumalizika Novemba, 2018 ambapo washindi watakuwa wamepatikana.

Tanzania inatakiwa kupambana na kuzishinda nchi za Cape Verde, Uganda na Lesotho katika kundi L ikiwa inataka kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika Cameroon mwaka 2019.

Katika droo iliyochezeshwa jana usiku jijini Libreville, Gabon, mbio za kusaka tiketi ya kufuzu fainali hizo zitaanza Juni mwaka huu na kumalizika Novemba, 2018 ambapo washindi watakuwa wamepatikana.

Mara ya mwisho Tanzania kufuzu fainali hizo ilikuwa mwaka 1980 nchini Nigeria ambapo wenyeji, Super Eagles, walitwaa kombe hilo kwa mara ya kwanza.

Kwa mujibu wa droo hiyo, mwanachama mwingine wa Cecafa, Rwanda imepagwa katika kundi H linaloundwa na nchi za Ivory Coast, Guinea na Jamhuri ya Afrika Kati.

Kenya itatakiwa kupambana vikali na majirani zake Ethiopia katika kundi F linalozijumuisha pia nchi za Ghana na Sierra Leone.

Burundi ipo kundi C ambalo linaundwa na mataifa ya Mali, Gabon na mshindi kati ya Djibouti au South Sudan.

Katika ukanda wa Afrika Mashariki, ni Uganda pekee iliyofuzu kushiriki michuano ya Afcon 2017 inayotarajiwa kuanza kesho nchini Gabon.

Droo kamili

KUNDI A: Senegal, Equatorial Guinea, Sudan, Sao Tome/Madagascar

KUNDI B: Cameroon, Morocco, Malawi, Comoros/Mauritius

KUNDI C: Mali, Gabon, Burundi, Djibouti/South Sudan

KUNDI D: Algeria, Togo, Benin, Gambia

KUNDI E: Nigeria, South Africa, Libya, Seychelles

KUNDI F: Ghana, Ethiopia, Sierra Leone, Kenya

KUNDI G: DR Congo, Congo, Zimbabwe, Liberia

KUNDI H: Ivory Coast, Guinea, Central African Republic, Rwanda

KUNDI I: Burkina Faso, Angola, Botswana, Mauritania

KUNDI J: Tunisia, Egypt, Niger, Swaziland

KUNDI K: Zambia, Mozambique, Guinea-Bissau, Namibia

KUNDI L: Cape Verde, Uganda, Tanzania, Lesotho