Tambwe ametumia dakika kibao

Amisi Tambwe

Muktasari:

  • Ngassa alifunga mabao matatu katika ushindi wa mabao 7-0 Yanga iliyopata dhidi ya Komorozine jijini Dar es Salaam kabla ya kufunga idadi kama hiyo pia kwenye mchezo wa marudiano nchini Comoro ambapo Yanga ilishinda kwa mbaao 5-2.

STAA wa zamani wa Yanga, Mrisho Ngassa alitumia dakika 180 tu za michezo miwili dhidi ya Komorozine ya Comoro kufunga mabao sita katika mashindano ya klabu Bingwa Afrika rekodi ambayo imemchukua staa wa timu hiyo Amissi Tambwe mechi 18 sawa na dakika 1,620 kuifikia.

Ngassa alifunga mabao matatu katika ushindi wa mabao 7-0 Yanga iliyopata dhidi ya Komorozine jijini Dar es Salaam kabla ya kufunga idadi kama hiyo pia kwenye mchezo wa marudiano nchini Comoro ambapo Yanga ilishinda kwa mbaao 5-2.

Wakati Ngassa akiwa tayari ameondoka klabuni hapo, straika Amissi Tambwe amelazimika kusubiri mechi 18 ili kufikia idadi hiyo ya mabao iliyowekwa na staa huyo ambaye anacheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini kwa sasa.

Tambwe aliichezea Yanga mechi sita katika mashindano ya kimataifa mwaka jana mechi mbili nyumbani na ugenini dhidi ya BDF IX ya Botswana, Platinum FC ya Zimbabwe na Etoile Du Sahel na kufunga mabao matatu.

Mwaka huu Tambwe ameicheza Yanga katika mechi 12 za mashindano hayo ya Afrika na kufunga mabao matatu pia ambayo ni dhidi ya Cercle De Joachims ya Mauritius, MO Bejaia na TP Mazembe