Sportpesa kuzikutanisha Yanga, Everton

Muktasari:

Mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Juni 5, mshindi wa kwanza ataibuka na kitita cha Dola 30,000.

Dar es Salaam. Kocha msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi amesema kwamba wanajifua kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya Ligi ya Sportpesa ambapo pia baadaye wana uhakika watakutana na Everton.

Mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Juni 5, mshindi wa kwanza ataibuka na kitita cha Dola 30,000.

Timu hiyo leo itashuka dimbani jijini Arusha kwenye mchezo wake wa kirafiki na AFC ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi za ligi hiyo.