Siri ya Wabongo kutimkia Oman yafichuka

Muktasari:

Kocha na mchezaji wa zamani wa Simba ambaye ni Muoman mwenye asili ya Tanzania, Talib Hilal amesema, mpira wa Oman kwa sasa uko juu na mshahara ni mkubwa, lakini wanawapa nafasi Wabongo baada ya kugundua kuna vipaji.

SIRI ya wachezaji wa Bongo kukimbilia Oman imefichuka na kwa waliopo, waamke kwa sababu kule kuna pesa hatari, mshahara wa Sh30mil sio ishu kabisa kwa waarabu.

Kocha na mchezaji wa zamani wa Simba ambaye ni Muoman mwenye asili ya Tanzania, Talib Hilal amesema, mpira wa Oman kwa sasa uko juu na mshahara ni mkubwa, lakini wanawapa nafasi Wabongo baada ya kugundua kuna vipaji.

Talib ameliambia Mwanaspoti kuwa, soka la huko limeibuka kwa kasi kutokana na matajiri wakubwa wa nchi hiyo kujitokeza na kumiliki klabu na kuwalipa wachezaji mkwara mrefu.

“Mpira wa Oman umekuwa na klabu zinamilikiwa na watu binafsi ndiyo maana mishahara imekuwa mikubwa sana.

Sehemu kubwa ya mastaa waliotamba Ligi Kuu Bara wametimkia huko akiwemo Mrisho Ngassa, Danny Lyanga wanaocheza Fanja, Elius Maguli wa Dhofar na Muivory Coast Kipre Tchetche.