Singida United yamkana Mnyarwanda

Wednesday April 19 2017

 

By Charles Abel, Mwananchi cabel@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Singida United imejiondoa katika mbio za kumsajili mshambuliaji wa Police FC, Danny Usengimana baada ya kushindwa dau lake la usajili.

Dau la mshambuliaji huyo Mnyarwanda ilivyoripotiwa na gazeti la The News Times la Rwanda, Faranga 8 milioni (sawa na zaidi ya Sh210 milioni) huku mshahara wake ukitajwa kuwa Sh 5 milioni kwa mwezi.

Licha ya mchezaji huyo kufichua mipango yake ya kujiunga na Singida United,  uongozi wa timu hiyo umekanusha suala hilo na kudai hawajazungumza nay

"Nimezungumza na viongozi wa Singida United na tumekubaliana kila kitu. Kisha wamefanya mazungumzo na uongozi wa timu yangu na kila kitu kimekwenda vizuri kilichobakia ni kusaini tu. 

Nilipata ofa kutoka timu nyingi, lakini nimeamua kukubali kwenda ligi ya Tanzania kwa sababu itasaidia kunijenga kisoka na kuwa njia ya kufikia mafanikio, " Usengimana aliliambia gazeti hili.

Katibu mkuu wa Singida United,  Abdulrahman Sima aliliambia gazeti hili kuwa taarifa zao wao kumalizana na mshambuliaji huyo sio sahihi.

"Ni taarifa tu ambazo vyombo vya habari vinaeneza lakini kiukweli sisi hatujafanya usajili wa huyo mshambuliaji wala kuzungumza naye kama ambavyo inasemwa

Majukumu yote ya usajili yapi mikononi mwa kocha Hans Pluijm ambaye kesho (leo)  atakutana na uongozi kuweka mikakati ya kuimarisha zaidi kikosi Chetu ambacho kimesajili wachezaji watatu tu wa kigeni ambao wanatoka Zimbabwe," alisema Sima.

Singida United tayari imesajili wachezaji watatu wa kigeni ambao ni Elisha Muroiwa na Wisdom Mtasa kutoka Power Dynamos pamoja na Tafadwa Kutinyu kutoka Chicken Inn zote zinashiriki Ligi Kuu Zimbabwe.

 

&&&&&&&&&&&&&