Simeone ajigamba mafanikio ya Atletico

Muktasari:

Timu hiyo kwenye mchezo wake wa awali ilipata sare ya bao 1-1 dhidi ya LeicesterCity, hivyo kutinga nusu fainali baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 yaliyowekwa nyavuni na Saul huku Jamie Vardy akifunga bao la kusawazisha kwa wenyeji.

Kocha wa Atletico Madrid, Diego Simeone amesema anaamini kikosi chache ni miongoni mwa klabu bora barani Ulaya kutokana na kutinga nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa juzi.

Timu hiyo kwenye mchezo wake wa awali ilipata sare ya bao 1-1 dhidi ya LeicesterCity, hivyo kutinga nusu fainali baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 yaliyowekwa nyavuni na Saul huku Jamie Vardy akifunga bao la kusawazisha kwa wenyeji.

Kocha Simeone alisema ni dhahiri timu hiyo imefikia kiwango cha Real Madrid na Barcelona pamoja na Bayern Munich.

ìUnapozungumzia kuhusu klabu kubwa barani Ulaya kiuchumi unazungumzia kuhusu Bayern Munich, Barcelona Real Madrid, lakini unapozungumzia  kuhusu mtazamo wa kisoka bila shaka tumefikia kiwango sawa.

ìNi jambo kubwa kufikia nusu fainali kwa mara ya tatu katika kipindi cha miaka minne nilichoitumikia klabu hii. Kwa mara ya kwanza nilipowasili klabuni hapa nilisema kwamba nitaka kuifanya Atletico  ilete ushindani kati ya timu tunazokutana nazo.

ìKwa sasa nimekuwa na furaha. Ninajivunia kiwango cha timu yangu na nina matumaini makubwa tutafika mbali kwenye mashindano haya.

Ushindi wa Atletico Madrid umeacha maumivu kwa Kocha Simeone baada ya wachezaji wake, Filipe  Luis na Juanfran kuwa majeruhi, huku akijigamba ataimaisha safu yake ya ulinzi ili kushinda michezo inayokuja.