Simba yashusha kifaa kipya

Muktasari:

MASHABIKI wa Simba kwa sasa wana kila sababu ya kutabasamu, baada ya mabosi wao kuonyesha wamepania kwelikweli, baada ya kushusha straika mwingine mpya kutoka Ghana, Diawou Johnson.

MASHABIKI wa Simba kwa sasa wana kila sababu ya kutabasamu, baada ya mabosi wao kuonyesha wamepania kwelikweli, baada ya kushusha straika mwingine mpya kutoka Ghana, Diawou Johnson.

Mchezaji huyo aliyetoka klabu ya Daraja la Kwanza nchini Ghana iitwayo,. Unit FC ameanza mazoezi jana jioni na Kocha Joseph Omog amesema atamuangalia kama anawafaa kabla ya kuwaambia mabosi wake, 'mpeni mkataba huyo'.

Simba ipo kambini mjini Morogoro na kesho Jumamosi itacheza mechi yake ya pili ya kirafiki dhidi ya KMC ya Daraja la Kwanza baada ya majuzi kuirarua Polisi Moro kwa mabao 6-0.