Simba yaomba kuandamana Dar

Muktasari:

Kwa mujibu wa barua ya Simba iliyosainiwa na rais wa Simba, Evance Aveva ilisema lengo la maandamano hayo ni kupeleka ujumbe kwa TFF ambayo imekuwa ikiwafanya uonevu katika uamuzi wa masuala mbalimbali ya klab hiyo.

Dar es Salaam. Uongozi wa Simba umeandika barua kwa Kamanda wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Simon Sirro ikiomba kufanya maandamano ya amani Jumanne ijayo kupiga uonevu wa Shirikisho la Soka TFF .

Kwa mujibu wa barua ya Simba iliyosainiwa na rais wa Simba, Evance Aveva ilisema lengo la maandamano hayo ni kupeleka ujumbe kwa TFF ambayo imekuwa ikiwafanya uonevu katika uamuzi wa masuala mbalimbali ya klab hiyo.

"Pia, tunazo taarifa kuwa msemaji wetu Haji Manara ameitwa katika kamati ya maadili kwa kile kinachoonekana kutaka kumfungia na kumziba mdomo ili asiweze kuzungumzia uonevu huo," ilisema barua hiyo. 

Maandamano hayo yataanza  saa 4:00 asubuhi hadi saa 7:00 mchana yakitokea makuu ya klabu hiyo kupitia barabara ya Msimbazi, Nyerere na Chang'ombe hadi Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo.