Simba yajifua Zanzibar

Muktasari:

Mratibu wa safari hiyo ya Simba, Abass Suleiman Ali alisema Tanzania ni kubwa ina maeneo mengi ya kujichimbia, lakini wanapendelea zaidi Zanzibar kutokana na utulivu wake.

Zanzibar. Vinara wa Ligi Kuu Bara, Simba wameanza kujifua asubuhi kwenye Uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar wakijiandaa na mechi dhidi ya Yanga.
Mratibu wa safari hiyo ya Simba, Abass Suleiman Ali alisema Tanzania ni kubwa ina maeneo mengi ya kujichimbia, lakini wanapendelea zaidi Zanzibar kutokana na utulivu wake.
Alisema wachezaji wanahitaji muda mzuri wa kupumzika pamoja na kupata hewa safi ili kujindaa vizuri kwa mechi, hivyo hali ya hewa ya Zanzibar inaweza kutimiza ndoto zao.
“Mbali ya hali ya hewa, lakini utulivu na masafa mafupi kutoka kambini hadi viwanjani nalo naona limezidi kutupa moyo wa kuelekeza makaazi ya muda visiwani hapa,”alisema.
Kikosi cha Simba kilinachojifua Zanzibar ni  Daniel Agyei, Peter Manyika, Denis Richad, Janier Bokungu, Hamad Juma, Mohamed Husein, Abdi Banda, Vicent Costa, Novaty Lufunga, Method Mwanjali, Jonas Mkude, James Kotei, Said Ndemla, Mohamed Ibrahi, Muzamil Yassin, Mwinyi Kazimoto, Shiza Kichuya, Jamal Mnyate, Laudit Mavugo, Pastory Athanas, Ibrahim Ajib, Hijja Ugando pamoja na Juma Luizo.