Simba yaanza kuweweseka

Wednesday April 19 2017

 

By Mwanasporti

Uongozi klabu ya Simba umesema hautakubaliana na uamuzi  ya kuwanyangíanya pointi tatu na Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi ya wachezaji ya Shirikisho la Kandanda Tanzania (TFF).

Afisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara amesema kuwa wamegundua njama za Kamati hiyo na viongozi wa TFF kuihujumu klabu yao hasa baada ya kamati ya masaa 72 kuinyangíanya ushindi timu ya Kagera Sugar baada ya kubainika kuwa ilimchezesha mchezaji Mohamed Fakhi huku akiwa na kadi tatu za njano.

Manara amesema kuwa Kamati  ya Sheria, Maadili na Hadhi ya wachezaji haina mamlaka ya kufanya marejeo ya maamuzi ya kamati ya Masaa 72 na kinachoendelea sasa ni hujuma dhidi yao. 

Ameushutumu uongozi wa Rais Jamal Malinzi na Katibu Mkuu, Mwesigwa Celestine kuwa wanatumia 'Uyanga waoí kwani wote hao wamewahi kuwa makatibu wakuu wa klabu hiyo kwa kipindi tofauti. 

Amesema kuwa hata serikali ilimtaka Malinzi ambaye na mwenyekiti wa chama cha soka cha mkoa wa Kagera kuachia nafasi moja kwani hata kwenye uamuzi huu, ameangalia maslahi ya mkoa wake.