Soka

Simba wakomaa na Kombe la FA

Share Bookmark Print Email
Email this article to a friend

Submit Cancel
Rating

By OLIPA ASSA  (email the author)
Email this article to a friend

Submit Cancel

Posted  Ijumaa,Aprili21  2017  saa 13:28 PM

Kwa ufupi;-

Meneja wa timu hiyo, Mussa Hassan ‘Mgosi’aliliambia Mwanaspoti kwamba ; “Simba ina programu zake tangu tulipoanza msimu huu, tunachokifanya ni muendelezo hivyo maandalizi yetu si ya kubagua timu, tunachokifanya atakayekuja mbele yetu ni kuhakikisha hatoki.”

LICHA ya Simba kutojua watacheza na nani nusu fainali ya Kombe la FA, wanachokiangalia ni kujifua ili timu itakayokuja mbele yao iambulie kipigo.

Meneja wa timu hiyo, Mussa Hassan ‘Mgosi’aliliambia Mwanaspoti kwamba ; “Simba ina programu zake tangu tulipoanza msimu huu, tunachokifanya ni muendelezo hivyo maandalizi yetu si ya kubagua timu, tunachokifanya atakayekuja mbele yetu ni kuhakikisha hatoki.”

“Hakuna mafanikio yanayokuja kirahisi, wachezaji wanajengwa kisaikolojia kujua namna ya kuishi wakati wa kilio, kicheko hapo ndipo wanaweza kustahimili na kutimiza ndoto zao kirahisi na siyo kuishi lele mama,”alisema.

Mgosi alisema wanapambana kuhakikisha msimu huu wanapeleka mataji mawili la Ligi Kuu Bara na Kombe la FA kwa sharti la kuwa na ushirikiano na kila mtu kusimamia majukumu yake kikamilifu.

“Viongozi wanafanya kazi yao ya kuhakikisha wachezaji wanakuwa na afya, kuwalipa mishahara yao, makocha wanafundisha mbinu za kila aina na wachezaji wanatakiwa kucheza kwa moyo,”alisema