Simba aipa Mbao mbinu za kuia Yanga

Muktasari:

Mbao itawakaribisha Yanga kwenye Uwanja CCM Kirumba katika mchezo wa nusu fainali ya pili ya Kombe la FA.

Mwanza. Winga wa zamani wa Coastal Union, Ahmed Simba amesema kama Mbao ikicheza katika kiwango kile walichokionyesha dhidi ya Simba hakuna ubishi kwamba wataitoa Yanga katika nusu fainali ya Kombe la FA itakayochezwa Jumapili.
Mbao itawakaribisha Yanga kwenye Uwanja CCM Kirumba katika mchezo wa nusu fainali ya pili ya Kombe la FA.
Winga Simba alisema Mbao ilionyesha soka safi katika mchezo wao dhidi ya Simba kama wakicheza hivyo Jumapili basi Yanga watafungwa.
Simba alisema kitu ambacho Mbao wanatakiwa kukifanya ni kuongeza umakini pekee haswa katika safu ya ulinzi katika mchezo huo.
Simba alisema licha ya Mbao kufungwa katika mchezo ule lakini walicheza soka safi ila walikosa umakini katika dakika za mwisho.