Siku za Rooney zahesabika

Muktasari:

Siku za Rooney katika kikosi cha England zimeanza kuhesabika baada ya kuachwa katika kikosi cha nchi hiyo kilichocheza na Ujerumani Jumatano iliyopita.

Gareth Southgate amekuwa akizungumza uwezekano wa Wayne Rooney kupewa mechi ya kuagwa kwenye Uwanja wa Wembley atakapostaafu.

Siku za Rooney katika kikosi cha England zimeanza kuhesabika baada ya kuachwa katika kikosi cha nchi hiyo kilichocheza na Ujerumani Jumatano iliyopita.

Rooney bado mechi sita tu aifikie rekodi ya Peter Shilton aliyoiweka kwa kuichezea England mechi125.
Mshambuliaji huyo wa Manchester United, Rooney (31), anataka kustaafu mwakani baada ya Kombe la Dunia la Russia, lakini sasa hali ni tofauti kwa sababu amepoteza namba katika klabu yake na timu ya taifa.

Pia, ameachwa katika kikosi kitakachocheza Jumapili mechi ya kusaka kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya Lithuania, hiyo ina maana matumaini yake ya kuichezea England 'Three Lions' kwenye Uwanja wa Wembley labda asubili hadi Septemba 4 wakati kikosi cha Southgate kitakapowakaribisha Slovakia.

Nyota wa Ujerumani, Lukas Podolski aliyeagawa Jumatano iliyopita jijini Dortmund alisema: “Naamini Rooney atapata mechi moja kubwa kwasababu yeye ni mchezaji bora wa England.

“Sijui kwanini hakucheza mechi hii au hakuwemo kwenye kikosi au ni utamaduni wa England kumpa nyota wake mechi bora.