Shomari Kapombe kurudishwa Sauzi

Shomari Kapombe

Muktasari:

  • Mwenyekiti mpya wa Azam, Nassoro Idrissa ‘Father’ alisema kwa mujibu wa taarifa ya daktari ni kwamba Kapombe alitakiwa kurejea Afrika Kusini ili kufanyiwa vipimo tena ambapo pia watampeleka beki wao Mghana, Daniel Amoah ambaye amekuwa akisumbuliwa na maumivu

AZAM FC inapanga kumrudisha beki wake wa kulia Shomary Kapombe nchini Afrika Kusini kwaajili ya kufanyiwa vipimo vya marudio kuona kama tatizo lake la awali limekwisha kabisa.

Mwenyekiti mpya wa Azam, Nassoro Idrissa ‘Father’ alisema kwa mujibu wa taarifa ya daktari ni kwamba Kapombe alitakiwa kurejea Afrika Kusini ili kufanyiwa vipimo tena ambapo pia watampeleka beki wao Mghana, Daniel Amoah ambaye amekuwa akisumbuliwa na maumivu.

Kapombe alipatiwa matibabu Afrika Kusini baada ya kugundulika kuwa damu ilikuwa imeganda katika mapafu na tayari alirejea uwanjani lakini Azam inataka kupata uhakika kama amepona kabisa.

“Kuhusu Kapombe ripoti inaonyesha kwamba alitakiwa kurejeshwa tena Afrika Kusini kwaajili ya checkup ili kuona kama alipona moja kwa moja.

“Huyu beki wetu Mghana Daniel Amoah naye ana maumivu chini ya tumbo, mwanzoni walidai ana maambukizi lakini inaonekana siyo sahihi, tumewasiliana na daktari wetu kule Afrika Kusini amesema pia tumpeleke,” alisema Father.