Shime kuzitumia Burundi, Ghana

Muktasari:

Serengeti Boys itacheza mechi mbili dhidi ya Burundi mjini Bukoba kabla ya kurejea Dar es Salaam na Aprili 3 itakapochuana na timu ya vijana ya Ghana.

Dar es Salaam. Kocha Mkuu wa Timu ya Vijana Serengeti Boys, Bakari Shime amesema atatumia mechi za kirafiki dhidi ya Burundi na Ghana kusoma mwelekeo wa kikosi chake.

Serengeti Boys itacheza mechi mbili dhidi ya Burundi mjini Bukoba kabla ya kurejea Dar es Salaam na Aprili 3 itakapochuana na timu ya vijana ya Ghana.

Shime alisema michezo hiyo ina umuhimu mkubwa wakati huu ikijiandaa na fainali za Afrika kwa vijana zitakazofanyika nchini Gabon.

Tumefanya mazoezi kwa muda na huu ni wakati wa kujipima tumefikia  wapi. Kama benchi la ufundi tunazipa kipaumbele kikubwa. Kabla ya kwenda Morocco lazima tujue nini tunapaswa kukifanyia kazi kwa bidii. Hizi ni mechi muhimu,î alisema kocha huyo aliyewahi kuinoa JKT Ruvu.

Serengeti itaweka kambi ya mwezi mmoja nchini Morocco kabla ya kwenda Gabon kushiriki fainali hizo za Afrika.

Daktari wa timu hiyo, Shecky Mngazija alisema afya za wachezaji zinaendelea vizuri na wote wapo tayari kwa mchezo huo.